MSHAMBULIAJI chipukizi, Lamine Yamal Nasraoui Ebana amesaini mkataba mpya wa muda mrefu kuendelea na kazi Barcelona ambao utamuweka kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2031.
Mkataba ambao japokuwa unaanza sasa, lakini Yamal atafikihsa umri wa miaka 18 Julai 13 na mchezaji huyo wa KImataifa wa Hispania anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi kama Robert Lewandowski.
Iwapo Yamal atacheza kwa kiwango cha juu na kumuwezesha kupata posho zote za kwenye mkataba wake mpya, basi malipo yake jumla pamoja na mshahara, posho na ada ya usajili itafikia Dola za Kimarekani Milioni 45.3 kwa mwaka kabla ya kukatwa kodi.
Kwa sababu hoyo, Yamal atakuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Barcelona, ingawa asilimia 50 ya hii italipwa kwenye kodi, kulingana na sharia za Hispania.
Pamoja na mafanikio yake msimu uliopita kwenye klabu na timu ya taifa, lakini hakuna wakati ambao mustakabali wa Yamal ulikuwa shakani Barcelona, kwani mchezaji huyo alitaka kubaki.
Mkataba wa awali Yamal ulisainiwa Oktoba 2023, akiwa ana umri wa miaka 16 wakati huo na kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuanza kwenye kikosi cha timu ya kwanza ya Barcelona akiwa tayari ameichezea timu ya wakubwa ya Hispania na kuifungia mabao na kuvunja rekodi mbili zaidi.
Mkataba wa 2023 ulikuwa una kipengele rasmi cha mchezaji huyo kuongeza mkataba akifikisha umri wa miaka 18 Julai 13 mwaka huu.
Kufuatia Yamal kufanya vyema kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya na kuiwezesha Hispania kutwaa Kombe hilo nchini Ujerumani – tetesi zikaibuka kutoka pande zote mbili, kwa mchezaji na klabu kwamba mkataba wake unapaswa kutazamwa upya.
0 comments:
Post a Comment