TIMU ya Crystal Palace imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester City leo katika mchezo wa Fainali Uwanja wa Wembley Jijini London.
Shujaa wa Crystal Palace leo ni mshambuliaji Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Eberechi Oluchi Eze aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 16 akimalizia kazi nzuri ya beki Mcolimbia, Daniel Muñoz Mejía.
Hilo linakuwa taji la kwanza rasmi kwa Crystal Palace kihistoria baada ya kulikosa mara mbili awali Runners-up: 1989–1990 na 2015–2016 mara zote wakifungwa na Manchester United katika Fainali.
Crystal Palace inakuwa klabu ya kwanza ya England kutwaa taji rasmi la kwanza baada ya Wigan Athletic msimu wa 2012-2013, Kombe la FA pia walipoifunga Manchester City pia kwenye Fainali.
0 comments:
Post a Comment