WENYEJI, RSB Berkane wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane nchini Morocco.
Mabao ya Berkane yamefungwa na kiungo Msenegal, Mamadou Lamine Camara kwa kichwa dakika ya nane akiunganisha kona iliyochongwa na beki Hamza El Moussaoui na mshambuliaji Oussama Lamlaoui la pili dakika ya 14 akimalizia pasi ya kiungo Imad Riahi.
Timu hizo zitarudiana Mei 25 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment