• HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2025

    PEDRO AIPOKONYA TONGE MDOMONI INTER MILAN, 2-2 NA LAZIO


    MSHAMBULIAJI mkongwe wa Kispaniola, Pedro Eliezer Rodríguez (37)Ledesma jana aliipokonya tonge mdomoni Inter Milan akiifungia Lazio bao la kusawazisha dakika ya 90 katika sare ya 2-2 kwenye mchezo wa Serie A Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan.
    Pedro alifunga pia bao la kwanza la Lazio pia, nalo likiwa la kusawazisha dakika ya 72 baada ya Inter Milan kutangulia na bao la beki Mjerumani Yann Aurel Ludger Bisseck mwenye asili ya Cameroon dakika ya 45'+2, kabla ya beki mwingine, Mholanzi, Denzel Justus Morris Dumfries kufunga la pili dakika ya 79.  
    Kwa matokeo hayo, Inter Milan inafikisha pointi 78 na inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Napoli baada ya wote kucheza mechi 37. Lazio inafikisha pointi 65 nafasi ya sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEDRO AIPOKONYA TONGE MDOMONI INTER MILAN, 2-2 NA LAZIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top