KLABU ya Yanga imesistiza haitacheza tena mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Simba hata kama itapangiwa tarehe mpya.
Taarifa ya Kamati ya Utendaji ya Yanga leo imesema kwamba hawana imani na Mamlaka za soka nchini, hivyo hawawezi hata kupeleka malalamiko yao kwenye mamlaka hizo.
Wiki iliyopita Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) ilisema kwamba itaupangia tarehe nyingine mchezo wa marudiano ya Ligi Kuu baina ya mabingwa hao watetezi, Yanga na mahasimu wao, Simba ambao uliahirishwa Machi 8, mwaka huu.
Taarifa ya TBLB ilisema Mei
1 kwamba hatua hiyo inafuatia Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kukataa kusikiliza kesi ya Yanga kutaka ipewe ushindi.

Mchezo huo uliingia mgogoro baada ya Simba kutishia kutoingiza timu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ilidai kuzuiwa kufanya mazoezi Machi 7, siku moja kabla ya mechi kwa mujibu wa kanuni.
Bodi ya Ligi ilitangaza rasmi kuuahirisha mchezo huo mchana wa Machi 8, lakini wakikwenda uwanjani na kufanya mazoezi kabla ya kuondoka na baadaye kufungua kesi CAS.
Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliitisha kikao na viongozi wa klabu zote, Bodi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ingawa haikuwahi kutoa majibu yoyote juu ya mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
0 comments:
Post a Comment