![]() |
Yondan akisaini Yanga. |
INADAIWA beki wa Yanga, Kevin
Yondan ametekwa na klabu yake ya zamani, Simba SC leo katika kile kinachoelezwa
jitihada za kumrudisha nyumbani.
Inadaiwa mchezaji wa zamani
wa Simba SC, ameongoza zoezi hilo la kumnasa Yondan na kumkutanisha na viongozi
wa Simba.
Yondan hakupatikana kwenye
simu yake alipotafutwa na BIN ZUBEIRY usiku huu, lakini Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb alipatikana na akasema; “Nipo nje ya
nchi, ila taarifa hizo ni kweli, lakini na sisi kwa ushirikiano wa mchezaji mwenyewe, tulifanikiwa kumkomboa mchezaji huyo na tumefungua kesi dhidi ya wahusika," alisema Bin Kleb.
0 comments:
Post a Comment