Katibu wa Azam, Nassor
Idrisa (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, kiungo wao mpya, Humphrey Mieno
waliyemsajili kutoka Sofapaka ya Kenya. Mieno ameungana na kikosi cha Azam
mjini hapa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako timu hiyo imekuja
kucheza Kombe la Hisani. Mieno alikuwepo kwenye kikosi cha Kenya, Harambee
Stars kilichofika fainali ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge wiki iliyopita na
kufungwa 2-1 na wenyeji Uganda, The Cranes. Amepewa jezi namba 30, ambayo iliwahi kuvaliwa
na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ aliyehamia SImba SC.
|