![]() |
Brandts akiwanoa wachezaji wake Uturuki |
Na Baraka Kizuguto, Antalya
Timu ya
Young Africans Sports Club kesho
itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa mwisho na wa tatu (3) dhidi ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza
nchini Uholanzi katika mchezo wa
kirafiki utakaofanyika katika viwanja vya Adora football - Berek pembeni kidogo
ya mji wa Antlaya.
Young
Africans ambayo imeshakaa takribani siku 12 katika mji wa Antalya na kucheza
michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Armini Bielefeld ya Ujerumani na
Denizlispor ya Uturuki leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya
Fame Residence football mjini Antalya.
Kocha Mkuu
wa Young Africans Ernest Brandts amesema atatumia mchezo huo wa mwisho kama
fursa pekee kwao kwani mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwao kwani timu ya
Emmen FC ni timu nzuri na ndio maana ipo katika ligi daraja la kwanza nchini
Uholanzi.
Akiongelea
mchezo huo wa kesho Brandts amesema timu
ya Emmen FC ni timu nzuri, imekuja Antalya kuweka kambi ya mafunzo kujiandaa na
mzunguko wa ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi, hivyo ni nafasi nzuri ya
kujipima uwezo na timu hiyo ya Uholanzi.
Young
Africans inatarajia kuondoka mjini Antalya siku ya jumapili mchana kupitia
Istambul ambapo itaondoka majira ya saa 1 usiku, saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki na inatarajiwa kufika Dar es salaam Tanzania majira ya saa 10 usiku
kasoro.