KOCHA Andre Villas-Boas amesema kwamba Tottenham ilimtumia ndege ya binafsi Emmanuel Adebayor ili awahi mechi dhidi ya Newcastle juzi, ambayo walishinda 2-1.
Adebayor aliwakera mashabiki wa Spurs wiki hii wakati alipochelewa kwa siku tano kurejea klabuni baada ya Togo kutolewa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, licha ya kwamba ni mshambuliaji pekee wa Spurs aliye fiti.
Villas-Boas alisema mapema wiki iliyopita kwamba anamataka Adebayor mazoezini Ijumaa, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliwasili saa 12:00 jioni ya siku hiyo na kukosa mazoezi, hivyo kutakiwa kukaa benchi katika mechi ya juzi, ingawa alichezeshwa.
Tottenham ilimtumia ndege Emmanuel Adebayor (kulia)
Njia pekee kwa Spurs kumrejesha haraka mchezaji wao Uingereza ilikuwa kumtumia ndege.
'Ndiyo, (tulimtumia ndege ikamchukue),' alisema kocha wa Spurs. 'Aliwasili Luton juzi majira ya saa 12 na kisha kuungana na timu hotelini.'
Kocha wa Spurs, Andre Villas alivutiwa na kiwango cha Adebayor
Villas-Boas ameendelea kuwa mpole anapoulizwa kuhusu kuchelewa kwa Adebayor.
Mreno huyo alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal alikuwa anashughulikia jambo baada ya timu yao kutolewa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika. Kama angekasirishwa na kitendo cha mchezaji huyo, asingeonyesha hadharani juzi.
'Kawaida, Ilikuwa vizuri kuwa naye,' alisema Villas-Boas, ambaye alimuingiza Adebayor uwanjani kipindi cha pili.
'Ameisaidia timu kupata matokeo mazuri, hivyo ni vizuri amerudi.
'Ni vigumu sana. Kwanza aliruhusiwa kurudi Ijumaa. Yakatokea mambo mambo yakamchelewesha, lakini bado aliwasili ndani ya muda na akafanya mazuri akitokea benchi.'
Adebayor alifanya kazi nzuri kwenye mechi hiyo akimsetia Gareth Bale kufunga bao la pili juzi.