Paul Gascoigne, picha hii alipoigwa katika tukio moja huko Northampton Januari 31, amekimbizwa kitengo cha wagonjwa walioo chini ya uangalizi maalum
MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa England, Paul Gascoigne amekimbizwa kwenye kitengo cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum, kabla ya kuanza kupata tiba za madhara ya ulevi.
Akiwa ana umri wa miaka 45, Gazza alishindwa kupata tiba katika kituo maalum, Rehab nchini Marekani alikopelekwa na kuibua hofu ya maisha yake.
Gascoigne alikuwa anaumwa taaban usiku wa Jumamosi, Gazeti la The Mail la leo limeandika, lakini hayuko kwenye hali ya hatari sana.
Mchezaji mwenzake wa zamani, Gary Lineker alisema rafiki yake anapambana.
Mwakilishi huyo wa Match of the Day ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: 'Gazza anapambana, acha tutumaini ataendelea kuwa huko.'
Nyota kadhaa walikwenda Marekani ambako wiki iliyopita ambako alitarajiwa kupatiwa tiba katika kliniki moja ya Tucson, Arizona.
Imeelezwa amepelekwa kwenye hospitali ya jirani ambako alipelekwa kwa siku nne zilizopita.
Kwa mujibu wa vyanzo, hali yake inandelea vema, ingawa haifahamiki lini haswa atakuwa tayari kiasi cha kutosha kuhudhuria kozi yake ya Rehab.
Kundi la marafiki zake watu maarufu, wakiwemo Chris Evans, Gary Lineker na Piers Morgan – wamelipia bili ya Gascoigne kuhudhuria kliniki hiyo, ambayo inagharimu pauni 30,000 kwa wiki nane za kuwa huko.
Tangu wakati huo, wachezaji kadhaa wa England, miongoni mwao Wayne Rooney, wameahidi kumchangia katika mfuko maalum.
Mchekeshaji James Corden pia amechangia fedha. Gascoigne alikubali kwenda Marekani baada ya kuona upendo wa mashabiki kwake, lakini wakati anawasili Arizona alipigwa picha akikata mvinyo wa Pint katika baa ya Uwanja wa Ndege, kabla ya rafiki zake kumkoponya.
Mchezaji wa zamani wa Tottenham Hotspur, Lazio na Newcastle United kwa kiasi kikubwa anatajwa kama mchezaji mwenye kipaji zaidi miongoni mwa wanasoka wa England.