Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika wamefika salama Dar es Salaam leo na jioni hii wameingia kambini katika hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Recreativo de Libolo ya Angola Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilibaki Arusha baada ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya JKT Oljoro, ambako iliendelea kujifua hadi leo wanarejea Jijini tayari kwa mchezo huo wa Jumapili. |