• HABARI MPYA

    Tuesday, February 12, 2013

    TFF YATAKA MASHABIKI WAJITOKEZA KUZISAPOTI AZAM NA SIMBA MICHUANO YA AFRIKA

    Azam

    Na Boniface Wambura
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linawataka mashabiki wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simba zitakazocheza mechi za mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.
    Nguvu ya washabiki ni muhimu katika kuziweza timu hizo kufanya vizuri katika mechi hizo za nyumbani dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Libolo ya Angola.
    Azam itacheza Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katika mechi ya Kombe la Shirikisho wakati Simba itaikabili Club Libolo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Jumapili. Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TFF YATAKA MASHABIKI WAJITOKEZA KUZISAPOTI AZAM NA SIMBA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top