KOCHA mpya wa Sunderland, Paolo Di Canio ameanza vibaya kazi baada ya kufungwa mabao 2-1 na Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jioni hii katika Ligi Kuu ya England.
Chelsea ilitoka uwanjani kwenda kupumzika ikiwa nyuma kwa bao 1-0 alilojifunga Cesar Azpilicueta dakika ya 45, lakini Matt Kilgallon naye akajifunga dakika ya pili ya kipindi cha pili akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Fernando Torres aliyetokea benchi kabla ya Branislav Ivanovic kuunganisha nyavuni shuti la David Luiz dakika ya 55 kuipatia Blues bao la ushindi.
Katika mchezo huo, kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel, Oscar, Mata/Lampard dk89, Hazard/Benayoun dk84 na Ba/Torres dk46.
Sunderland; Mignolet, Bardsley, Kilgallon, O'Shea, Rose, N'Diaye, Gardner/Colback dk82, Larsson/McClean dk71, Sessegnon, Johnson na Wickham.
Mwanzo mbaya: Di Canio amepoteza mechi ya kwanza kazini Sunderland leo
Furaha: Oscar (katikati) na Eden Hazard wakishangilia bao la kusawazisha la Chelsea
Katika mechi nyingine, Liverpool imelazimishwa sare ya bila kufungana nyumbani na West Ham United, wakati Tottenham Hotspur imetoka sare ya 2-2 na Everton.
Bao la dakika za lala salama (dakika ya 87) la Gylfi Sigurdsson ndilo limeinusuru Tottenham kupata kipigo kingine leo.
The Toffees walionekana kabisa kuwa katika nafasi ya kushinda leo, baada ya Phil Jagielka (dakika ya 15) na Kevin Mirallas (dakika ya 53)kutangulia kufunga, kufuatia Emmanuel Adebayor kuifungia Spurs dakika ya kwanza tu.
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akikwepa kiatu cha beki wa West Ham, James Collins (kushoto)


.png)