KLABU ya Real Madrid imepunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa La Liga, Barcelona hadi 10 wakati Gonzalo Higuain, Kaka na Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil waliotokea benchi walipoifungia mabao katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Levante.
Kocha Jose Mourinho aliwaacha benchi mastaa wake kadhaa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kwenda kulinda ushindi wake wa 3-0 mbele ya Galatasaray Jumanne katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Bao na busu: Cristiano Ronaldo alinenepesha ushindi wa Real Madrid dhidi ya Levante
Akiwaonyesha ishara ya busu mashabiki


.png)