![]() |
| Samatta kushoto akiwa na Mputu; wote walifunga jana na sasa watamenyana na Pirates |
Na Prince Akbar
KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imefanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya jana kuifunga Mochudi Centre Chiefs ya Botswana mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Stade du TP Mazembe mjini Lubumbashi.
Kwa matokeo hayo, Mazembe imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 7-0, baada ya awali kushinda 1-0 wiki mbili zilizopita ugenini, bao pekee la Mtanzania, Mbwana Samatta.
Mazembe sasa itamenyana na Orlando Pirates ya Afrika iliyoitoa Zanaco ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-1. Ikishinda 1-0 ugenini na 2-1 nyumbani jana.
Mabao ya Mazembe jana yalifungwa na Rainfrod Kalaba dakika ya sita na 35, Tressor Mputu dakika ya 15 na 80, Samatta dakika ya 75 na Eric Nkulukuta dakika ya 90.
Mbali na Samatta, katika kikosi cha Mazembe kuna Mtanzania, mwingine, Thomas Ulimwengu ambao wote wanafanya vizuri kwa sasa na pia ni tegemeo la nchi yao katika kampeni za kwenda Brazil 2014.



.png)