MPANGO wa kocha Arsene Wenger kumnyakua Mario Gotze atue Arsenal umeingia kiza baada ya wakala wa kiungo huyo wa Borussia Dortmund kusema hana mpango wa kuhama mwishoni mwa msimu huu.
Vyanzo vya habari vimesema kocha wa Gunners, amekosa kifaa kutokana na mpango wa nyota huyo kutaka kujiunga na Barcelona baada ya msimu mmoja zaidi Westfalenstadion.
Msaidizi wa zamani wa Wenger Arsenal, David Dein, alisema klabu yake hiyo ya zamani ina orodha ndefu ya wachezaji inayotaka kuwasajili na Jumapili BIN ZUBEIRY ikaripoti kwamba Gotze ni mchezaji aliyekuwa nafasi za juu kwenye orodha hiyo.
Chini kabisa utakuta video ya mavitu ya Gotze
Haondoki: Gotze (katikati) anaonekana kutaka kubaki
VIDEO Gotze akifanya vitu adimu Dortmund