MSHAURI wa zamani wa vigogo wa Ufaransa, Paris St Germain amesema klabu hiyo itamsajili Wayne Rooney kutoka Manchester United mwishoni mwa msimu.
Licha ya kocha wa United, Sir Alex Ferguson kusema hivi karibuni kwamba Rooney hataondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu, mwanasoka huyo wa kimataifa wa England, ameendelea kuhusishwa kuhamia kwa matajiri wa Ufaransa, PSG.
Sasa, Michel Moulin – ambaye alifanya kazi kwa muda mfupi kama mshauri wa PSG mwaka 2008 – amesema mpango wa Rooney kutua huko upo na utatimia.
Anakawenda Ufaransa: Wayne Rooney ameripotiwa kuwa mbioni kuhamia Ligue 1 kuichezea Paris Saint-Germain
Kifaa kitang'oka: Rooney amekuwa akiichezea Manchester United tangu mwaka 2004 alipojiunga nayo akitokea Everton