KLABU ya Manchester United ilimshuhudia Radamel Falcao akiifungia mabao mawili Atletico Madrid Jumapili usiku na inafahamika Sir Alex Ferguson anamtaka mshambuliaji huyo.


BIN ZUBEIRY ilinadika wiki iliyopita kwamba Ferguson anataka kutumia Pauni Milioni 47 - ambazo zitahusisha na kubadilishana na Javier Hernandez ili kumnasa mkali huyo wa mabao wa Colombia.
Wakati United inashinda 2-0 dhidi ya Stoke, Ferguson alimpeleka msaka vipaji wake mkuu, Jim Lawlor kumuangalia Falcao akifunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 nyumbani dhidi ya Granada.
Kaangalie video chini
Anatakiwa: Radamel Falcao (kushoto) akiichezea Atletico Madrid ikiifunga Granada
Manchester City na Chelsea zote nazo zimehusishwa kwa kiasi kikubwa kuwania saini ya Falcao, ambaye amejijengea jina kama mmoja wa wapachika mabao hodari duniani, kwa kuifungia mabao 56 Atletico tangu ajiunge nayo akitokea Porto mwaka 2011.
Lakini United imepiga hatua kubwa katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ikijiandaa kumuacha Hernandez ahamie Madrid kama sehemu ya dili hilo.
Anaondoka? Javier Hernandez akiichezea United dhidi ya Stoke Jumapili, lakini anaweza kuondoka
VIDEO Angalia mabao bora ya Falcao