KLABU ya Juventus imepiga hatua kubwa katika mbio za uibingwa wa Italia, Serie A baada ya jana usiku kujitania kileleni kwa pointi 11 zaidi kufuatia mabao mawili ya Arturo Vidal kuwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya Lazio.
Vidal aliwafungia Juve kwa penalti baada ya Lorik Cana kumuangusha Claudio Marchisio kwenye eneo la hatari dakika ya nane.
Mkwaju nyavuni: Arturo Vidal akifunga kwa penalti
Siku za furaha: Vidal akishangilia na Claudio Marchisio na Stephan Lichtsteiner
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Chile, Vidal alifunga bao la pili dakika 20 baadaye akimalizia pasi ya Mirko Vucinic.
Ikiwa imebakiza mechi sita, Juve ina pointi 74 wakiiacha mbali Napoli katika nafasi ya pili. AC Milan yenye pointi 59 ni ya tatu.
"Ushindi huu ni muhimu sana sana kwa kutuwezesha kuzidi kupiga hatua kuelekea kwenye ubingwa,"alisema kocha Antonio Conte.
"Bado tunahitaji pointi saba na hatutazungumza hadi tumbebe mwali,"aliongeza.
La pili: Vidal akiifungia Juventus bao la pili