KLABU za Chelsea na Manchester City za England zinamfuatilia mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani, Mario Gomez.
Klabu zote hizo za Ligi Kuu England zinamtaka sana mpachika mabao wa Napoli ya Italia, Edinson Cavani, huku City ikifahamika kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumtwaa. Timu itakayokosa saini ya nyota huyo wa Ujerumani, Gomez, na Bayern ikiwa tayari kusikiliza ofa zitakazokuja kwa ajili ya mchezaji wao huyo mwenye umri wa miaka 27, itahamishia mawindo yake huko.
Wakala Uli Ferber amesema: "Mario hafurahishwi na mambo kwa sasa,".
Hana furaha: Mario Gomez (kushoto) anaweza kuondoka Bayern Munich
Namba 1: Chelsea na Manchester City zote zitapenda saini ya Edinson Cavan kwanza