MSHAMBULIAJI Wayne Rooney anataka mazungumzo ya mkataba mpya Manchester United mwishoni mwa msimu na amewaambia rafiki zake, hayuko tayari kuondoka Old Trafford kuhamia Paris St Germain.
Mpachika mabao huyo wa United jana ilielezwa na Mshauri wa zamani wa PSG nchini Ufaransa kwamba dili la kumhamishia klabu ya Paris liko vizuri.
Pamoja na hayo, inafahamika kwamba, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kukaa chini na United mwishoni mwa msimu huu kujadili kuongezewa mkataba ambao bado una miaka miwili.
Enlarge
Atabaki au ataondoka: Wayne Rooney anataka kubaki Old Trafford, lakini taarifa zinasema anatakiwa PSG
Majadiliano na klabu hiyo ambayo muda si mrefu itavishwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England yanatarajiwa kuwa mazito.
Rooney hatakuwa na shaka ya kuendelea kulipwa mshahara wa sasa wa Pauni 200,000 kwa wiki tangu Oktoba 2010 na United inaweza kumuongezea maslahi kidogo katika mkataba mpya.