![]() |
| Tom Cruise akifuarahia Guinness |
Na Princess Asia
GUINNESS imemkaribisha katika zulia jekundu mmoja wa nyota wakubwa wa fiamu duniani, mwigizaji Tom Cruise katika jumba la Guinness Storehouse mjini Dublin, Ireland wiki iliyopita.
Cruise, aliungana na nyota wengine kama Rais wa Marekani, Barrack Obama ambaye alionekana akifurahia Guinness sehemu mbalimbali hivi karibuni, ikiwemo katika siku ya St Patrick.
Cruise aliwasili Dublin Jumatano iliyopita katika sehemu ya ziara yake ya kuipromoti filamu yake ya sasa, Oblivion aliyoshirikiana na mwongoza filamu ‘baab kubwa’, Joseph Kosinski na kimwana wa zamani wa Bond, Olga Kurylenkoe.
Tangu kufunguliwa kwake mwaka 2000, Guinness Storehouse imepokea wageni zaidi ya Milioni 9 kutoka sehemu mbalimbali duniani na ni sehemu inayoongoza kwa mvuto kwa wageni Ireland.
![]() |
| Anajipimia; Tom Cruise akijimiminia Guinness |




.png)