• HABARI MPYA

    Sunday, May 05, 2013

    AZAM FC YAFUNIKA TUZO YA MWANASOKA BORA TANZANIA, YANGA NAYO KWA WA WACHEZAJI WA KIGENI YAPOTEZA

    Khamis Mcha 'Vialli' wa Azam anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania

    Na Prince Akbar
    AZAM FC imeingiza wachezaji wawili katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) 2012/2013 ambao ni Khamis Mcha ‘Vialli’ na John Bocco ‘Adebayor’.
    Katika kipengele hicho, nyota hao wawili wa Azam watachuana na Kevin Yonda wa Yanga, Shomary Kapombe wa Simba anayeshikilia tuzo hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wote wa TP Mazembe ya DRC. 
    Azam imeingia mchezaji mmoja katika kipengele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kigeni anayecheza Tanzania, ambaye ni Kipere Herman Tchetche kutoka Ivory Coast atakayechuana na Mganda Emmanuel Okwi aliyekuwa Simba kwa sasa ameuzwa Etoile du Sahel ya Tunisia.
    Katika kipengele hiki, Yanga SC imeingiza wachezaji wawili ambao ni Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
    Upande wa wanasoka wa kike, Fatuma Mustafa atachuana na Asha Rashid, Mwanahamisi Omary, Sofia Mwasikili anayeshikilia tuzo huyo na Esther Chabruma.
    Katika mpira wa magongo wanaume Sylvester Kigodi atachuana na Castor Mayuma, Gurtej Bilu Singh, Vendri Bhamra na Elias Samala. Gofu ya Kulipwa; Hassani Kadio, Yassin Salehe, Fadhili Nkya, Salimu Mwanyenza na Rajabu Iddy.
    Gofu Ridhaa wanawake; Madina Iddi, Angel Eaton, Hawa Wanyeche, Ayne Magombe na gofu ya Ridhaa wanaume, Jimmy Mollel, Frank Roman, Nuru Mollel, Martin MacDonald na John Said.
    Katika ngumi za Ridhaa wanaume; Ismail Isack Galiatano, Said Hofu, Selemani Kidunda, Victor Njaiti na Mohamed Chibumbui na kwa wanawake, Sara Andrew, Irene Kimaro, Easther Kimbe, Mather George na Mariam Nyerere.
    Ngumi za Kulipwa; Francis Miyeyusho, Ramadhan Shauri, Thomas Mashali, Said Mbelwa na Francis Cheka. Judo Bara Wanaume; Ahmed Magogo, Andrew Mlugu, Geoffrey Mtawa, Gervas Chilipweli, Abuu Mcheteko na Abubakar Nzige. Judo Wanawake Bara;  Matrida Temba, Amina Mohamed.
    Judo Zanzibar Wanaume; Mohamed Khamis Juma, Masoud Amour Kombo na Mbarouk Suleiman wakati kwa wanawake visiwani humo ni Grace Alphonce na Laylati Mohamed. Katika Tenisi wanawake ni Rehema Athumani, Vailety Peter, Mkunde iddi, Edna John na Zuhura Baraka wakati kwa Wanaume ni  Omary Abdallah, Yassin Shaaban, Hassan Kassim, Kiango Kipingu na Lebric Jacob. 
    Mpira wa Mikono Wanaume; Faraji Shaibu, Hemedi Salehe, Abinery Kusena, Ally Khamis na Hassan Yussuf wakati kwa wanawake ni Catherine Mapua, Dorris Mangara, Zakia        Mohamed, Happy Mahinya na Mary Kimiti.

    Katika Riadha wanawake, Zakia Mrisho atachuana na Mary Naali, Jaqckueline Sakilu, Sarah Ramadhani, Anjelin Tsere na Sarah Maja wakati kwa wanaume Dickson Marwa atachuana na Faustine Mussa, Augstino Sule, Bazil John na Samson Ramadhan.
    Kriketi Wanaume Abhik Patwa atachuana na Benson Mwita, Seif Khalifa, Issa Kikasi na Riziki Kiseto na kwa wanawake, Monica Paschal atachuana na Mwanaidi Ibrahim, Hadija Nassib, Esther Wales, Mwanaidi Ammy na Mary Waya wa Filbert Bayi pekee, aliyekuwa kocha mchezaji. 
    Kikapu Wanawake Faraja Malaki atachuana na Evodia Kazinja, Sajida Ahmed, Rehema Kilomba na Tukusubira David na kwa wanaume, Mussa Chacha atapambana na Lusajo Samuel, Salim Mchemba, Filbert Mwaipungu na Steven Atanasio.
    Katika Netoboli, Lilian Sylidion atachuana na Mwanaidi Hassan, Irene Elias Kanile, Jacqueline Sikozi na Faraja Malaki.
    Kwa upande wa wachezaji bora chipukizi, katika soka Salum Abubakari ‘Sure Boy’ wa Azam atachuana na Frank Domayo wa Yanga na Edward Cristopher wa Simba kwa upande wa soka.
    Katika Tenisi ni Emmanuel Malya wa Gymkhana Arusha, Tambwe Juma kwa Kriketi.
    Mwanasoka Bora Anayecheza Nje, tuzo hiyo itashindaniwa na Ulimwengu na Mbwana Samatta wa TP Mazembe ya DRC, Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya, Hasheem Thabeet wa Oklahoma, Soud Abdulrazak na Ramadhani Abdallah ‘Dulah’ wanaocheza kikapu Uganda
    Kama kawaida, tuzo ya heshima itatangazwa ukumbini siku ya utoaji wa tuzo hizo. 
    Majina ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa kupata majina.
    Pia vyama viwili vya michezo ya  paralimpiki na baiskeli bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu pia kimeshindwa kuwasilisha majina.
    Hatua ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.
    Awali TASWA ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja na chama kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika tarehe itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.
    “Tunavishukuru vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho,”alisema Mwenyekiti wa Kamati, Hajji Manara.
    TASWA itatoa tuzo kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo  Katibu wake ndiye pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha wanastahili, ambapo baadaye washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa Mwaka 2012.
    Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka ya karibuni ni Mwanaidi Hassan (2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle (2007) na Samson Ramadhan (2006).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM FC YAFUNIKA TUZO YA MWANASOKA BORA TANZANIA, YANGA NAYO KWA WA WACHEZAJI WA KIGENI YAPOTEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top