BONDIA Floyd Mayweather Jnr ametoka gerezani na kuendeleza ubabe katika ndondi kwa kushinda pambano la uzito wa Welter dhidi ya Robert Guierrero kwa pointi.
Robert Guerrero alishindwa pointi 117-111 zilizotolewa na majaji wote waliompa ushindi Mayweather.
Katika pambano hilo, Mayweather alipoteza raundi ya pili tu kwa pointi 119-109.
Wengi walikuwa wana wasiwasi baada ya Mayweather kutoka jela angeathirika kimchezo, lakini usiku wa jana alikuwa moto mkali.
Bado bingwa: Floyd Mayweather amerejea ubingwa wake wa Welter baada ya kumpiga kwa pointi Robert Guerrero