![]() |
Bao la 17; Seif Abdallah na Erasto Nyoni wakimpongeza Kipre Tchetche |
Na Mahmoud Zuberiy, IMEWEKWA MEI 12, 2013 SAA 11:55 JIONI
AZAM FC imekata rasmi tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ushindi huo, unaifanya Azam itemize pointi 51, sita nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye 57 kila timu ikiwa imebakiza mechi moja kumaliza ligi.
Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na John Raphael Bocco dakika ya 23 kufuatia kazi nzuri9 ya Humphrey Ochieng Mieno.
Kipindi cha pili, Azam tena walirudi na kasi nzuri na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 lililofungwa na Kipre Herman Tchetche baada ya kuichambua ngome ya wapinzani na kupioga shuti mariadi.
Hilo lilikuwa bao lake la 17 msimu huu hivyo kujihakikishia ufungaji bora wa Ligi Kuu, akiritihi mikoba ya Bocco ‘Adebayor’, ambaye naye alimrithi Mrisho Khalfan Ngassa akiwa Azam pia kabla ya kutolewa kwa mkopo Simba SC.
Joackins Otieno Atudo aliunganishwa kwa kichwa kona ya Erasto Edward Nyoni dakika ya 80 na mpira ukatinga nyavuni na hata kipa Tonny Kavishe alipojaribu kuuokolea ndani, lakini ukagonga nyavu za juu na kudondokea ndani tena, hilo likiwa bao la tatu katika mchezo wa leo.
Azam sasa watacheza tena michuano ya Shirikisho mwakani, baada ya mwaka huu kutolewa Raundi ya Tatu na AS FAR Rabat ya Morocco wakishiriki kwa mara ya kwanza.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam
Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk85, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Abdi Kassim dk83 na Brian Umony/Seif Abdallah dk63.
JKT Mgambo; Tony Kavishe, Salum Mlima, Ramadhani Malima, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Mussa Gunda, Juma Mwinyimvua/Peter Mwalyanzi dk 56, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.