IMEWEKWA MEI 11, 2013 SAA 3:50 ASUBUHI
DILI la Wayne Rooney kuuzwa kwa Pauni Milioni 25 Chelsea limepata upinzani kufuatia taarifa kwamba, Bayern Munich wanataka pia kumsajili mshambuliaji huyo wa Manchester United.
Wana fainali hao wa Ligi ya Mabingwa, Bayern wanataka kupambana na kocha anayetaka kuhama Real Madrid, Jose Mourinho na kwenda kuweka kambi tena Stamford Bridge na kuhakikisha Rooney anakuwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili.
Lakini BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail imegundua kwamba vyanzo vya ndani kutoka Allianz Arena vimepuuzia nia yoyote ya kumtaka mpachika mabao huyo wa Manchester United, hivyo kutoa mwanya wa Chelsea kumnasa kiulaini akaanze maisha mapya.
Anaondoka? Wayne Rooney anaweza kuondoka Manchester United baada ya miaka tisa