• HABARI MPYA

    Tuesday, May 07, 2013

    DIDIER DROGBA AENDELEA KUTAMBA ULAYA AKIIWEZESHA GALATASARAY KUTWAA TAJI LA 19 UTURUKI


    KLABU ya Galatasaray imetwaa taji la 19 la ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki, baada ya kuifunga Sivasspor mabao 4-2 mjini Istanbul.
    Mabao mawili kila mtu ya Selcuk Inan na Burak Yilmaz yaliipa timu ya Fatih Terim ushindi dhidi ya Sivasspor, ambayo mabao yake yalifungwa na  Kadir Bekmezci na Cihan Ozkara.
    Ushindi huo, unafuatia kipigo cha Fenerbahce cha mabao 2-0 kutoka kwa Istanbul BB, ambao sasa wanazidiwa mara moja idadi ya kutwaa mara nyingi ubingwa nchi hiyo, kwani wao wametwaa mara 18.
    Aidha, ushindi huo unamfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba atwae taji lingine katika nchi nyingine.
    Substantial: The champions have a 10-point lead at the top of the table with two games left to play
    Mabingwa kwa pointi 10 zaidi kileleni zikiwa zimebaki mechi mbili
    Drogba alicheza tangu mwanzo hadi mwisho, lakini kiungo Wesley Sneijder, aliyesajiliwa kutoka Inter Milan ambaye kama ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, alicheza saa moja tu.
    Nyota Yilmaz, amefikisha mabao 21 msimu huu, na sasa Galatasaray inaongoza ligi kwa pointi 10 zaidi zikiwa zimebaki mechi mbili.
    Bragging rights: Bitter rivals Fenerbahce have won 18 titles
    Wapinzani wao wakubwa, Fenerbahce wametwaa mataji 18
    Fans favourite: Didier Drogba is among Galatasaray's key players
    Kipenzi cha mashabiki: Didier Drogba ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Galatasaray
    Kocha Terim Terim alifungiwa mechi tisa Aprili kwa kumbwatukia refa katika mechi ya ligi dhidi ya Mersin Idmanyurdu na hakuwepo kwenye benchi timu yake ikisherehekea ushindi huu kwa kutumikia adhabu yake.
    Mastermind: Fatih Terim is Galatasaray's coach
    Mzee wa mipango: Fatih Terim ni kocha wa Galatasaray
    Target man: Drogba remains capable of playing at the highest level
    Anayelengwa: Drogba bado anaokota mafanikio Ulaya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DIDIER DROGBA AENDELEA KUTAMBA ULAYA AKIIWEZESHA GALATASARAY KUTWAA TAJI LA 19 UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top