• HABARI MPYA

    Tuesday, May 07, 2013

    MAMBO YAMEIVA MISS TANGA 2013


    Na Princess Asia
    MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" yanaanza leo kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Entertainment, Asha Kigundula, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri.
    Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miss Tanga 2012 Theresia Kimolo na Mwanaidi Omar.
    Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo.
    Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya  warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.
    "Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula.
    Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
    Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari, Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.
    Shindano hilo limedhaminiwa na Redd's, CXC Africa& Tours, Tanga Beach Resorts, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Cloud's Media Group, pamoja na Blog za Bin Zubeiry, Michuzi Media Group, Saluti5, Kajuna, JaneJohn, na Kidevu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAMBO YAMEIVA MISS TANGA 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top