
Mwanadada msanii chipukizi wa temeke akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vya zhakem - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii
Na Prince Akbar
KUNDI maarufu la Bongo Fleva, likiongozwa na kinara wake, Sir Nature mwishoni mwa wiki lilipambana tamasha la Airtel Yatosha katika viwanja vya mbagala Zakhem katika siku za jumamosi na Jumapili, ambalo liilifana.
Walikuwepo pia wasanii wengine maarufu, likiwepo kundi la Tip Top Connection, chini ya kiongozi wake, Madii, kundi la wakali wa dansi pamoja na wasanii mbalimbali wakiwemo Ney wa Mitego na Roma Mkatoliki.
Akizungumzia tamasha hilo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema; “Tumeweza kushuhudia burdani kabambe kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wasanii wa kizazi kipya na wasanii chipukizi wa Temeke katika viwanja vya Zakhem. Lakini pia mbali na burdani, wateja wa Airtel wameweza kuunganishwa na huduma ya Airtel yatosha na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na faida zake, wateja waliweza kujiunga na kusajili namba zao”.
"Tunawashukuru watanzania na wateja wetu wote waliojitokeza kwa wingi kupata burdani hii na tunawahaidi kuendelea kuwapa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kutanua wigo wa mawasiliano nchini aliongeza "Mmbando
Huduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama poa ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.pamoja muda wa maongezi mteja anapata vifurushi vya kutuma ujumbe mfupi na internet na vifurushi hivi vinapatikana kwa siku au kwa wiki, ili kujiunga na huduma hii piga *149*99# ufurahie huduma poa na ujionee "Airtel Yatosha"