• HABARI MPYA

    Sunday, May 12, 2013

    MANCINI ALIFUKUZWA HATA KABLA YA MECHI YA WIGAN JANA

    IMEWEKWA MEI 12, 2013 SAA 4:10 USIKU
    MUDA wa Roberto Mancini kuwa kocha wa Manchester City dhahiri umekwisha.
    Mtaliano huyo atafukuzwa wakati wowote kuanzia sasa nafasi yake ikichukuliwa na kocha Mchile, anayeinoa Malaga kwa sasa nchini Hispania, Manuel Pellegrini mara tu City itakapomalizana naye.
    Inafahamika Mancini anaweza kutupiwa virago hata usiku wa leo au kesho asubuhi na hana uhakika wa kukaa kwenye benchi usikuwa Jumanne kuiongoza timu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Reading.
    Time's up: Roberto Mancini's spell as Manchester City manager will be ended this week
    Muda umefika: Roberto Mancini anafikia tamati ya kufanya kazi Manchester City wiki hii
    New man: Manuel Pellegrini is set to leave Malaga and take over Mancini's job at the Etihad
    Mtu mpya: Manuel Pellegrini anajiandaa kuondoka Malaga na kurithi mikoba ya Mancini Etihad

    REKODI KAMILI YA MANCINI MAN CITY

    Ligi Kuu England:
    Mechi 133, Kushinda 82, Sare 27, Kufungwa 24.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 61.7 
    Kombe la FA:
    Mechi 19, Kushinda 13, sare tatu, kufungwa tatu.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 68
    Kombe la Ligi:
    Mechi tisa, kushinda nne, sare moja, kufungwa nne.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 44.4
    Ligi ya Mabingwa:
    Mechi 12, kushinda tatu, sare nne, kufungwa tano.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 25 
    Europa League:
    Mechi 16, Kushinda 10, sare tatu, kufungwa tatu.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 62.5 
    Ngao ya Jamii:
    Mechi mbili, kushinda moja, kufungwa moja.
    Asilimia ya ushindi: Asilimia 50 
    Jumla:
    Mechi 191, kushinda 113, sare 38, kufungwa 40.
    Asilimia ya ushindi : Asilimia 59.2 
    Uamuzi huo umechukuliwa na vigogo watatu wa City: Ferran Soriano, Txiki Begiristain na Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak kabla ya kipigo cha jana kwenye fainali ya Kombe la FA dhidi ya Wigan.
    Hata ushindi katika mechi hiyo usingeweza kunusuru ajira yake.
    Mancini amebakiza miaka mitatu katika mkataba wake mpya aliosaini baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini atalipwa mafao yake, mamilioni ya Pauni kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia.
    Mtaliano huyo inafahamika leo alikuwa hotelini London mchana na asiyejali lolote kuhusu mustakabali wake.
    Pia inafahamika kwamba Mancini hafukuzwi kwa sababu ya matokeo mabaya, bali mahusiano yake mabovu na wengine katika klabu.
    Begiristain na Soriano wote wamekuwa hawaridhishwi na tabia ya Mancini katika chumba cha kubadilishia nguo.
    Lakini pia namna ambavyo kocha huyo amekuwa akiwananga viongozi wa klabu hiyo kwenye vyombo vya habari, nayo pia inatajwa kama sababu inayochangia kitumbua chake kuingia mchanga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MANCINI ALIFUKUZWA HATA KABLA YA MECHI YA WIGAN JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top