IMEWEKWA OKTOBA 13, 2013 SAA 11:50 ALFAJIRI
PAMOJA na kwamba Lionel Messi alishindwa kucheza jana kutokana na kusumbuliwa na maumivu, lakini haikuzuia Barcelona kushinda 2-1 dhidi ya Atletico Madrid usiku wa jana na kushangilia taji la 22 la Ligi Kuu Hispania.
Messi alianza katika mechi ya kwanza ndani ya raundi sita kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja la kulia, lakini akaondoka uwanjani dakika ya 68 Barcelona ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Radamel Falcao dakika ya 52 na Barca ikakamilisha wachezaji wote watatu wa kubadilisha.
Hata hivyo, Alexis Sanchez akasawazisha dakika ya 72 na kiungo wa Atletico, Gabi Fernandez akajifunga dakika ya 80 hivyo kuamsha pati la ubingwa kwa Barcelona, wakiivua rasmi ubingwa Real Madrid.
Mabingwa: Wachezaji wa Barcelona wakishangilia taji la La Liga
La ushindi jioni: Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya Lionel Messi kutoka
Heshima: Atletico Madrid wakiwapa heshima yao wachezaji wa Barcelona kwa kuwa mabingwa, wakati wanaingia uwanjani
Barcelona inaweza kufikisha rekodi ya Madrid msimu uliopita kufikisha pointi 100 kama itashinda mechi zake tatu zilizobaki.
Atletico itamenyana na Madrid katika fainali ya Kombe la Mfalme Ijumaa. Wakati huo huo, beki wa Real Madrid, Raphael Varane amesema atahitaji upasuaji wa goti lake la kulia.
Atletico itamenyana na Madrid katika fainali ya Kombe la Mfalme Ijumaa. Wakati huo huo, beki wa Real Madrid, Raphael Varane amesema atahitaji upasuaji wa goti lake la kulia.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29 aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter jana. Varane aliumia mguu huo katika sare ya 1-1 na Espanyol Jumamosi, ambayo iliihakikishia Barcelona ubingwa.
Washindi: Nyota wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas na Alex Song wakishangilia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Barcelona
Aliwanyima raha kwa muda: Radamel Falcao akishangilia bao lake
Matawi ya Juu: Barca walitoka nyuma kushinda mechi yao ya 29 msimu huu
Mapema siku hiyo, Valencia ilijiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Roberto Soldado alifunga mabao mawili kabla ya mapumziko, wakati Andres Guardado na Nelson Valdez wakakamilisha karamu ya mabao kipindi cha pili.
Huo ulikuwa ushindi wa pili mfululizo wa 4-0 kwa Valencia na unamaanisha timu ya Ernesto Valverde inaizidi kwa pointi moja Real Sociedad, ambayo leo itakuwa mwenyeji wa Granada.
Malaga na Sevilla zote zina nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya baada ya sare ya bila kufungana uwanja wa La Rosaleda.
Glum: Manuel Pellegrini, anayejiandaa kuhamia Manchester City, alishuhudia sare ya bila kufungana na Malaga na Sevilla