• HABARI MPYA

    Sunday, May 12, 2013

    PAUL SCHOLES ATUNGIKA DALUGA ZAKE KIMOJA LEO

    IMEWEKWA MEI 12, 2013 SAA 5:45 ASUBUHI
    KIUNGO Paul Scholes amethibitisha kustaafu kwa mara pili.
    Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa England alistaafu kwa muda mwaka 2011 lakini akarejea kazini Manchester United January mwaka jana.
    Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza leo dhidi ya Swansea tangu alipocheza mara ya mwisho Januari, anafikiri ni wakati mwafaka kutungika daluga.
    "Ndiyo, hatimaye natungika daluga zangu moja kwa moja,"alisema.
    Winding down: Paul Scholes will retire for the second time having been little more than a bit part player
    Paul Scholes atastaafu kwa mara ya pili leo
    Paul Scholes
    "Kucheza soka ndiyo kitu pekee nimekuwa nikitaka kufanya na nimekuwa na muda mrefu na wa mafanikio Manchester United, chini ya kocha babu kubwa daima, imekuwa heshima,"alisema.
    Scholes anayepewa heshima ya mchezaji bora wa kizazi chake na wachezaji wa timu pinzani na timu yake pia, atacheza mechi yake ya 498 ya Ligi Kuu England leo, maana yake atakuw amekaribia kutimiza mechi 500.
    Kwa ujumla amecheza mechi 716 akiwa na Mashetani Wekundu na alifunga bao lake la mwisho katika mabao yake 155 dhidi ya mabingwa wa Kombe la FA, Wigan Septemba mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PAUL SCHOLES ATUNGIKA DALUGA ZAKE KIMOJA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top