• HABARI MPYA

    Sunday, May 12, 2013

    RASMI BARCA MABINGWA LA LIGA, REAL YAWANIA JAPO TAJI MMOJA IJUMAA


    IMEWEKWA MEI 12, 2013 SAA 5:55 ASUBUHI
    KAMA ilivyotarajiwa, Barcelona imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania usiku wa jana baada ya washindani wao wakuu, Real Madrid kushindwa kuwafunga Espanyol kwenye Uwanja wa Estadi Cornella-El Prat.
    Mabingwa watetezi, Madrid walihitaji ushindi nyumbani kwa wapinzani wa Jiji wa Barca kuendelea kumsubirisha kocha Tito Vilanova na vijana wake kusherehekea ubingwa, lakini wakalazimishwa sare ya 1-1.
    Matokeo hayo yanaifanya Barca iongoze La Liga kwa pointi saba zaidi wakijiandaa kucheza na Atletico Madrid leo, huku kikosi cha Jose Mourinho kikiwa kimebakiza mechi mbili kumaliza msimu wa ligi.
    Super sub: Cristiano Ronaldo came off bench to rescue Real Madrid
    Super sub: Cristiano Ronaldo alitokea benchi na kuisawazishia Real Madrid
    Out of sorts: Real Madrid's Kaka struggled to make an impact
    Kaka wa Real Madrid akiwatoka watu
    Pure delight: Barcelona celebrate regaining the La Liga title from Real Madrid
    Mashabiki wa Barcelona wakishangilia jana taji la La Liga baada ya Real Madrid kuchemsha
    The party starts: Thousands of Barcelona fans came out to celebrate winning the league
    Hii ni mara ya nne katika miaka mitano Barca kutwaa taji hilo na mara ya 22 kwa ujumla - wakizidiwa mara 10 na wapinzani wao wa jadi, Madrid.
    Na pia ni taji la kwanza kwa kwa Barca chini ya kocha mpya Vilanova, ambaye alifungwa na Madrid katika kuwania Super Cup ya Hispania mwanzoni mwa msimu na kutolewa katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich na Kombe la Mfalme dhidi ya Madrid.
    Vilanova, ambaye wiki hii alirejea New York alikokuwa anatibiwa saratani kwa miezi miwili mapema mwaka huu, alipandishwa kutoka timu ya vijana kurithi mikoba ya Pep Guardiola aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
    Solemn bunch: The Real Madrid bench
    Benchi la Real Madrid
    Waiting game: Subs Ronaldo, Iker Casillas and Karim Benzema
    Walipumzishwa: Ronaldo, Iker Casillas na Karim Benzema benchi

    Espanyol, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Christian Stuani dakika ya 23 na Hector Moreno alifunga bao ambalo lilikataliwa wakati Real ina nafasi ya kutwaa taji moja, itakapomenyana na Atletico Madrid katika Fainali ya Kombe la Mfalme Ijumaa.
    Hata hivyo, Cristiano Ronaldo alitokea benchi na kusawazisha dakika ya 58 kufuatia kazi nzuri ya Gonzalo Higuain.
    Espanyol ilipoteza mchezaji mmoja dakika za majeruhi wakati Victor Sanchez alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Higuain, lakiini mpira wa adhabu uliopigwa na Ronaldo ulipaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RASMI BARCA MABINGWA LA LIGA, REAL YAWANIA JAPO TAJI MMOJA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top