![]() |
Chaz Baba katikati, kushoto Nyoshi na kulia Ferguson |
Na Asha Said
BENDI ya muziki wa Dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma, inatarajia kusindikiza uzinduzi wa Albamu ya mpya ya Bendi ya Mashujaa itakayokwenda kwa jila la Risasi Kidole.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii katika ukumbi wa Bissines Park Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wanamuziki wanaokubalika kwa sasa katika tasnia hiyo Chaz Baba (Mashujaa) na Nyosh El Sadat wa FM.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Chaz Baba ambaye ni Rais wa Mashujaa alisema, wamejipanga vya kutosha katika uzinduzi huo na ndio sabau kubwa ya kuwaomba FM kuwasindikiza ikiwa ni lengo la kuwapa burudani mashabiki wao.
“Tumejipanga sana, kutoa burudani nzuri nay a uhakika kwa wadau na mashabiki wetu watakaouzulia siku hiyo, kwani uzinduzi huo sio wa kitoto njooni mjionee wenyewe,”alisema Chaz.
Aidha Chaz aliongeza kuwa, albam hiyo inatarajiwa kuwa na nyimbo tisa huku huku akijitamba Raper wake kama Fergason kufanya makamuzi ya ajabu siku hiyo.
Naye Nyoshi alisema, kutokana na utu walionao na upendo ndiyo sababu iliyowafnaya kukubali ombi la Mashujaa nkuwasindikiza katika uzinduzi huo, na kudai kuwa siku za usoni hata wao wanatarajia kuwa na uzinduzi wa albam mpya huenda wakawaalika hata wao.