• HABARI MPYA

    Friday, June 07, 2013

    BREAKING NEWS; CHELSEA YAANZA MAZUNGUMZO NA NAPOLI KUHUSU CAVANI...YAINGIA KWA VITA NA REAL MADRID KUWANIA SAINI YA JOVETIC

    IMEWEKWA JUNI 7, 2013 SAA 1:30 ASUBUHI
    MSAKO wa Chelsea kwa washambuliaji umeshika kasi baada ya jana usiku kuanza mazungumzo na mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 50, Edinson Cavani wa Napoli, saa kadhaa baada ya kutoa ofa ya Pauni ya Milioni 34.9 kumnasa mshambuliaji wa Zenit St Petersburg, Hulk.
    Kocha Jose Mourinho ameorodhesha wachezaji wanne anaowataka wakiwemo kutoka Fiorentina, Stevan Jovetic na Manchester City, Edin Dzeko katika orodha hiyo.
    Interest: Napoli have opened talks with Chelsea over Uruguay striker Edinson Cavani (left)
    Napoli imeanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani (kushoto)
    Mourinho anajiamini atamsajili mchezaji wa Pauni Milioni 25, Jovetic na kuwapiku Juventus, lakini anakabiliwa na ushindani kutoka klabu yake ya zamani, Real Madrid katika kuwania saini ya Cavani wakati Dzeko anaonekana kuwa mboni mbadala. Napoli haijakataa mpango wa kubadilishana Cavani na Dzeko na Manchester City, lakini mpango unaonekana kusinzia.
    Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis alisema jana usiku: "Kuna dhamira kutoka Chelsea kwa Cavani, watanipigia mimi saa chache zijazo. Nitafurahi akibaki, lakini ikiwa ataondoka atampata mbadala wake,".
    Mshambuliaji wa Brazil, Hulk pia amethibitisha Mourinho anamtaka Stamford Bridge.
    Target: Chelsea have made a £35m offer for Zenit St Petersburg's Brazilian forward Hulk
    Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 35 kwa Zenit St Petersburg juu ya Mbrazil, Hulk.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BREAKING NEWS; CHELSEA YAANZA MAZUNGUMZO NA NAPOLI KUHUSU CAVANI...YAINGIA KWA VITA NA REAL MADRID KUWANIA SAINI YA JOVETIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top