• HABARI MPYA

    Monday, July 08, 2013

    RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMMED SHEIN AZINDUA GATI MPYA YA MALINDI ILIYOJENGWA NA BILIONEA BAKHRESA

    IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 6:00 MCHANA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Sheikn akizundua jiwe la Msingi la Gati mpya ya Malindi, Zanzibar asubuhi ya leo. Nyuma yake ni mmiliki wa makampuni ya S.S.B., Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa, ambaye amejenga Gati hiyo kwa ajili ya matumizi ya boti zake za Azam Marine na nyingine zote zinazofanya safari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar na Zanzibar na Pemba. 

    Uzinduzi

    Dk. Shein akisalimiana na Mzee Bakhresa alipowasili eneo la Gati hiyo ya kisasa 

    Hapa sasa safi kabisa; Mzee Bakhresa akimuongoza Dk. Shein kujionea sehemu mbalimbali za Gati hiyo

    Mzee umefanya jambo kubwa na la heri; Dk. Sheik akizungumza na Mzee Bakhresa katika meza kuu wakati sherehe za uzinduzi wa Gati hiyo

    Anamwaga wino; Dk. Shein akisaini kitabu cha wageni wa Azam Marine pembeni ya Mzee Bakhresa

    Kwenda chini; Mzee Bakhresa akimuelekeza jambo Dk. Shein na msafara wake wakati akikagua gati hiyo

    Twende kule ukaone zaidi; Mzee Bakhresa akimuongoza Dk. Shein

    Si unaona mwenyewe; Mzee Bakhresa akimuelekeza kitu Dk. Shein

    Tuanzie kule; Mzee Bakhresa na Dk Shein

    Nimekubali Mzee; Dk Shein akijionea uzuri wa Gati mpya...Mzee Bakhresa kulia

    Watoto hawa walitoa burudani nzuri wakati wa sherehe za uzinduzi wa Gati

    Utamaduni; Wakicheza ngoma ya asili

    Vibinti vya Kizenji; Watoto wa kike nao walitoa burudani

    Mzee Bakhresa akiwa na Mkuu wa Idara ya Ulinzi ya S.S.B., Abood Mzee Mbwana katika Lounge ya VIP ya Gati hiyo 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMMED SHEIN AZINDUA GATI MPYA YA MALINDI ILIYOJENGWA NA BILIONEA BAKHRESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top