• HABARI MPYA

    Sunday, July 07, 2013

    YANGA SC WABUNGE WAIFUMUA SIMBA SC NA KUTWAA KOMBE LA MATUMAINI MBELE YA RAIS JK


    Wabunge wa Yanga wameng'ara Taifa leo dhidi ya watani Simba SC
    Na Elius Kambili, IMEWEKWA JULAI 7, 2013 SAA 12:55 JIONI
    TIMU ya Yanga SC ya Wabunge, imetwaa ubingwa wa Tamasha la Matumaini baada ya kuwafunga Wabunge wa Simba kwa penalti 4-3 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii, kufuatia sare ya bila kufungana.
    Rais Kikwete akianzisha mchezo
    Kipa hodari kwa michomo ya penalti wa Simba SC, Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan leo aligeuzwa shati tu langoni baada ya kutunguliwa penalti zote zilizopigwa na Wabunge wa Yanga.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kupuliza kipenga Rais Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kupuliza kipenga Waliofunga penalti za Yanga ni Michael Kadebe, Mark Tanda, Christopher Kabenyele na Said Mtanda, wakati kwa Simba Yona Kilumbi alipaisha ya kwanza, Amos Makala, Adam Malima na Abel Kigula wakafunga zilizofuata na Aziz Abood akakosa ya tano.

    Rais Kikwete akielekea kukagua timu.
    Rais Kikwete akisaini mpira utakaotumika.
    ...Akiwakagua Yanga.

    ..Akiwakagua Simba.
    Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Eric Shigongo, Waziri Fenella Mukangara, marefarii na manahodha wa Simba na Yanga.
    Vikosi vya Simba na Yanga.
    JK akipuliza kipenga.

    Mtanange ukiendelea.
    Score board ilisomeka hivi.
    Mashabiki.
    Kipa wa Yanga, Hussein Zubeiry Mbunge wa Fuoni Zanzibar alisimama imara leo kulinda lango Yanga na kuokoa michomo mingi ya hatari.
    Mechi hiyo ilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliyeanzisha kabla ya kumuachia refa Athumani Kazi aendelee. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SC WABUNGE WAIFUMUA SIMBA SC NA KUTWAA KOMBE LA MATUMAINI MBELE YA RAIS JK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top