• HABARI MPYA

    Friday, August 16, 2013

    CHELSEA KUMSAJILI ETO'O WAKIMKOSA ROONEY

    IMEWEKWA AGOSTI 16, 2013 SAA 7:43 MCHANA
    KLABU ya Chelsea bado ina dhamira ya kumsajili mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala, Samuel Eto'o.
    The Blues kwa sasa wanataka straika, staa wa Manchester United, Wayne Rooney ndiyo chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho.
    Eto'o alishinda ligi ya mabingwa akiwa na Inter Milan mwaka 2010 akicheza chini ya Mourinho. 
    Seeking a move: Samuel Eto'o is keen on leaving Anzhi Mackhachkala, with Chelsea a possible destination
    Anataka kuondoka: Samuel Eto'o amepania kuondoka Anzhi Mackhachkala na Chelsea ikipewa nafasi ya kumnasa.
    Mapema wiki hii gwiji huyo wa Cameroon alikiri kwamba anataka kucheza chini ya kocha wa Chelsea.
    Alisema: “Kuna Jose Mourinho mmoja tu. Nimecheza chini ya makocha wengi wazuri – lakini hakuna mwenye tabia kama za Jose.
    “Ni mmoja kati ya makocha bora duniani – na tulifanikiwa sana tulipokuwa pamoja Inter Milan. Ningependa kucheza chini yake tena – kwa sababu huchoki kuwa pembeni ya Jose.
    “Ndio Chelsea ni timu bora – na tutakapopata ofa zote mezani, hapo nitazungumza na wakala wangu na kujua hatua yangu nyingine.”
    Hatahivyo, Dynamo Moscow wamewasajili wachezaji wenzake Igor Denisov, Yuri Zhirkov na Aleksandr Kokorin.  
    On his way out: Former Chelsea defender Yuri Zhirkov (left) has left Anzhi for Dynamo Moscow
    Anasepa: Staa wa zamani wa Chelsea, Yuri Zhirkov (kushoto) ameondoka Anzhi na kutua Dynamo Moscow.
    Italian job: Jose Mourinho led Inter Milan to the Champions League title in 2010, with the help of Eto'o
    Mzigo wa Italia: Jose Mourinho aliiongoza Inter Milan kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010 kwa msaada wa Eto'o
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA KUMSAJILI ETO'O WAKIMKOSA ROONEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top