Na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 16, 2013 SAA 1:30 MCHANA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ili kufanya uamuzi wenye manufaa kwa washabiki wa mpira wa miguu baada ya tarehe ya uchaguzi aliyotangaza kuingilia na mechi ya watani wa jadi (Simba na Yanga) ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Sekretarieti ya TFF imepokea maoni kutoka kwa wapenzi mbalimbali wa mpira wa miguu wakiomba matukio hayo mawili (Uchaguzi wa TFF na mechi ya Simba na Yanga) yafanyike katika siku tofauti.
Wakati Kamati ya Uchaguzi inatangaza uchaguzi kufanyika Oktoba 20 mwaka huu tayari ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa imeshatoka, na ikionesha kuwa timu ambazo zina historia ya kipekee katika mpira wa miguu zitacheza siku hiyo.
Sekretarieti imelazimika kumwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kwa vile yeye na kamati yake ndiye wenye mamlaka ya kuitisha Mkutano wa Uchaguzi. Huko nyuma TFF imeshafanya mikutano huku kukiwa na mechi za timu ya Taifa (Taifa Stars), jambo ambalo liliwezekana kutokana na mikutano hiyo kuwa na ajenda moja tu.
Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni ameitisha kikao cha kamati yake kujadili barua hiyo ya sekretarieti.
Wakati huo huo: Tiketi kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam itakayochezwa kesho (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitaanza kuuzwa saa 3 asubuhi.
Vituo vitakavyouza tiketi hizo Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Barber Shop iliyoko Sinza Madukani.
Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari yote yanayouza tiketi yatahamia uwanjani saa 7 kamili mchana.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.

![]() |
Simba na Yanga; Viungo Athumani Iddi 'Chuji' wa Yanga kushoto na Amri Kiemba wa Simba kulia katika mechi iliyopita watani. Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa siku moja na mechi hii. |