IMEWEKWA AGOSTI 15, 2013 SAA 1:12 ASUBUHI
ENGLAND jana imewafunga wapinzani wao, Scotland, mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Wembley.
Mabao ya England yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 29, Danny Welbeck dakika ya 53 na RickieLambert dakika ya 70, Scotland ilitangulia kupata mabao yake kupitia kwa Morrison dakika ya 11 na Miller 49.
Kikosi cha England kilikuwa Hart, Walker, Cahill, Jagielka/Jones dk84, Baines, Cleverley/Milner dk67, Gerrard/Oxlade-Chamberlain dk62, Wilshere/Lampard dk46, Walcott/Zaha dk75 na Rooney.
Scotland: McGregor, Hutton, Martin, Hanley, Whittaker, Snodgrass/Conway dk66, Morrison/Rhodes dk82, Brown, Forrest/Mulgrew dk67, Maloney/Naismith dk86, Miller/Griffiths dk73.
Rickie Lambert akiifungia bao la ushindi England
Lambert akishangilia na Frank Lampard baada ya kufunga
Rooney akipambana na alisababisha bao la ushindi lililofungwa na Lambert
Rooney akigeuka kutoka upande wa mashabiki wa Scotland
James Morrison akifumua shuti kumtungua Joe Hart
Shuti la Morrison likielekea moja kwa moja nyavuni
Kitu nyavuni
Majanga:... na Hart anashuhudia nyavu zake zinatikisika
Unaikumbuka hii? Mchezaji wa zamani wa Scotland, Gordon McQueen akiifungia nchi yake katika Uwanja huo huo mwaka 1977
Theo Walcott akielekea kufunga akiwa ndani ya eneo la penalti
Baada ya kumtoka beki, Walcott alifumua shuti hadi nyavuni
Bonge la bao...mambo ya Walcott
Asante Theo! Tom Cleverley akimkumbatia winga wa Arsenal baada ya kufunga
Kenny Miller akiifungia Scotland
Gary Cahill...
Miller akishangilia baada ya kuwapa wapinzani wa England bao la kuongoza
La kusawazisha: Danny Welbeck aliisawazishia England
Welbeck amefunga bao la sita tangu aanze kuichezea England
Wachezaji wa England akiwemo Wayne Rooney (katikati) wakishangilia bao la kusawazisha la Welbeck
Rooney akiondoka kinyonge uwanjani.
KWA MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZOTE ZA KIRAFIKI JANA, SHUKA CHINI KABISA YA UKURASA
KWA MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZOTE ZA KIRAFIKI JANA, SHUKA CHINI KABISA YA UKURASA