IMEWEKWA AGOSTI 15, 2013 SAA 1:42 ASUBUHI
KLABU ya Manchester United itafanya jaribio lingine la mwisho katika harakati za kuinasa saini ya Cesc Fabregas kutoka Barcelona ikiwa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania atakosa namba mwanzoni mwa msimu katika timu hiyo ya Nou Camp.
United ineokana bado kuwa na nia na Fabregas licha ya mchezaji huyo kusema wiki iliyopita kwamba anataka kubaki katika klabu yake ya sasa. "Tunaheshimu uamuzi wa Cesc,"ilisema United.
Jaribio la mwisho: Manchester United itapeleka ofa ya mwisho kwa ajili ya Cesc Fabregas licha ya yeye mwenyewe kusema anataka kubaki
Hakati tamaa: Tayari ofa mbili za Moyes zimepigwa chini
Pamoja na hayo, BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba United inaendelea kufuatilia mazingira ya Fabregas na itakuwa tayari kurejea tena na ofa ya mwisho ya Pauni Milioni 32 iwapo kiungo wa zamani wa Arsenal ataanzia benchi msimu wa La Liga.
Fabregas hatacheza mechi ya ufunguzi ya Barcelona dhidi ya Levante Jumapili baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mechi ya kirafiki nchini Malaysia mwishoni mwa wiki na hatarajiwi kuwa fiti ndani ya muda.
Mtaalamu wa pasi: Fabregas hana uhakika kama atapata namba kikosi cha kwanza mbele ya Xavi (kushoto) na Andres Iniesta
Hata hivyo, anatarajiwa kuwa fiti Jumatano kwa ajili ya Super Cup dhidi ya Atletico Madrid na atakuwa na mechi nyingine nne kabla ya dirisha la usajili la majira haya ya joto kufungwa mwishoni mwa Agosti.
Katika mechi hizo tatu, United watamuangalia. Moja ya sababu zinazomfanya kocha wa United, David Moyes aamini Fabregas ataondoka Nou Camp ni kutokuwa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mbele ya Xavi na Andres Iniesta katika safu ya kiungo ya Barcelona.
Ofa mbili za United zimekwishapigwa chini, ya pili ikiwa ni rekodi katika historia ya usajili ya klabu, Pauni Milioni 31, mwezi mmoja uliopita.
Fabregas kwa sasa ni majeruhi