• HABARI MPYA

    Thursday, August 15, 2013

    KIIZA ATIMKIA LEBANON JUMAPILI, YANGA WATOA BARAKA ZOTE AENDE

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 15, 2013 SAA 6:25 MCHANA
    MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mganda Hamisi Friday Kiiza atacheza mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini Jumapili atapanda ndege kwenda Lebanon, kufanya majaribio ya kujiunga na klabu moja ya huko.
    Kiiza atakwenda Lebanon kwa baraka za uongozi wa klabu yake, Yanga SC, kwani klabu hiyo inayomtaka imefuata taratibu.
    Taji la mwisho? Hamisi Kiiza akiwa na Kombe la ubingwa wa Bara aliloshinda na Yanga SC mwishoni mwa msimu

    Habari kutoka Yanga SC, zimesema kwamba timu ya Lebanon imetoa ofa nzuri kwa timu ya Jangwani kwa ajili ya Kiiza, lakini kwanza imetaka imfanyie majaribio na kumpima afya ndipo hatua nyingine zifuate.
    Inaelezwa ni ofa nzuri ambayo imewalainisha Yanga SC na wameridhia kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda, aliyewasumbua mno kusaini Mkataba mpya majira haya ya joto.
    Tayari Kiiza amekwishaitumikia Yanga SC kwa miaka miwili, akiiwezesha kutwaa mataji mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na moja la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Na akiwa katika siku za mwanzo kabisa za Mkataba wake mwingine wa miaka miwili aliosaini hivi karibuni, linakuja jaribio la kusitisha maisha yake Jangwani.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KIIZA ATIMKIA LEBANON JUMAPILI, YANGA WATOA BARAKA ZOTE AENDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top