IMEWEKWA AGOSTI 16, 2013 SAA 12:40 JIONI
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amerejea mazoezini kikosi cha kwanza Manchester United kabla ya mechi ya kwanza ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea.
Rooney aliichezea England ikishinda wa 3-2 dhidi ya Scotland Jumatano, alionekana yuko fiti na tayari kufanya kazi kwenye kikosi cha David Moyes katika mechi ya kwanza ya ushindani.
Mshambuliaji huyo bado anahusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford, huku wapinzani wa United katika Ligi Kuu, Chelsea wakiwa mstari wa mbele kutaka kumsajili.
VIDEO Nenda chini kuangalia Gerrard akimzungumzia Rooney
Amerudi: Wanye Rooney akiwasili mazoezini Manchester United leo asubuhi
Nyuma ya kioo: Mustakabali wa Rooney bado haueleweki, akihusishwa kutimkia Chelsea
Amehusishwa kwenye kikosi cha David Moyes kuelekea mchezo huo, lakini Rafael na Javier Hernandez wote majeruhi wa nyama za paja na mawinga waili, Nani na Ashley Young wanatarajiwa kuwa nje.
Wilfried Zaha anajiandaa kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu, wakati Michael Carrick anatarajiwa kupona maumivu ya jichos aliyoyapata akiichezea England mechi ya kirafiki.
Rooney amekuwa nje ya kikosi cha United wakati wa kujiandaa na msimu kutokana na maumivu ya bega, na baada ya kumuona akiichezea nchi yake, Moyes amemjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu, huku akisistiza hauzwi.
"Hakuna maendeleo zaidi na hatutaki chochote, kwa sababu tumekwsihamuambia kila mtu hauzwi," alisema Moyes.
"Nitahitaji kuona, yukoje atakaporejea. Nitajaribu na kumfautilia. Nimeona mchezo usiku wa juzi, nafikiri kwa dakika 65 alizocheza alifanya vizuri, anazunguka na anaonekana yuko fiti.'
Hatimaye kazini...: Wayne Rooney alicheza mechi yake ya kwanza wakati wa kujiandaa na msimu, England ikishinda dhidi ya Scotland
Kwenye kipaza: Kocha wa United, David Moyes anasistiza Rooney hauzwi