IMEWEKWA OKTOBA 7, 2013 SAA 3:02 USIKU
TANGU kustaafu kwa Lennox Lewis hajatokea mbabe mwingine mwenye mvuto katika ndondi za uzito wa juu, lakini Jumamosi usiku Anthony Joshua alionyesha anaweza kurudisha raha katika masumbwi ya uzito wa juu.
Mbabe huyo wa London na mshindi wa Medali ya Dhahabu ya Olimpiki, alianza vyema ndondi za kulipwa kwa kumpiga mpinzani wake Emanuele Leo kwa Knockou (KO) Raundi ya kwanza ukumbi wa O2 Arena.
Chali, kwisha kazi : Anthony Joshua (kushoto) akiwa amemdondosha Emanuele Leo katika Raundi ya kwanza kwenye pambano lake la kwanza la ndondi za kulipwa
Tayari anatabiriwa kuwa Lennox Lewis mwingine na kutamba katika ulimwengu wa ndondi hadi kuwa bingwa asiyepingika wa uzito wa juu duniani.
Kazi nyepesi: Joshua alianza vyema maisha ya ndondi za kulipwa
Ana ngumi nzito
Anatisha kijana: Joshua atarejea ulingoni baadaye mwezi huu ili kujijenga zaidi
Mwisho, konde la nguvu la Joshua limetua kichwani kwa jamaa