NAHODHA John Terry amempa raha kocha Jose Mourinho, kwa kuipa Chelsea ushindi wa 3-2- akifunga mabao mawili dhidi ya timu ya Daraja la pili, AFC Wimbledon.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ilikuwa nyuma zikiwa zimesalia dakika 16 kutokana na kazi nzuri ya Ade 'The Beast' Akinfenwa, lakini kuingia kwaTerry na Branislav Invanovic kulibadilisha matokeo.
The Blues ilidondoshwa na mabao ya Alan Bennett kwa kichwa dakika ya 40 kabla ya Matt Tubbs kumtungua kwa penalti, Mark Schwarzer.
Terry alipunguza bao la kwanza na Mohamed Salah akasawazisha zikiwa zimesalia dakika saba kabla ya Nahodha JT kufunga la ushindi.

Super sub: John Terry akienda hewani kuifungia Chelsea bao la ushindi dhidi ya AFC Wimbledon Uwanja wa Kingsmeadow
Terry akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la ushindi
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Schwarzer/Beeney, Zouma/Terry, Ake/Ivanovic, Christiansen/Chalobah, Bamford/Da Silva, Baker, Aina/Brown, Salah, Van Ginkel/Houghton, Swift/Romeu na Matic/Solanke.


.png)
0 comments:
Post a Comment