WABRAZIL wawili wapo mazoezini Yanga SC kwa zaidi ya wiki sasa, kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Santana Santos ‘Jaja’.
Wamekuja baada ya klabu hiyo kuajiri makocha Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva.
Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinataka wachezaji watano tu wa kigeni na kabla ya Wabrazil hao, Yanga tayari ina beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote wa Rwanda na washambuliaji Hamisi Kiiza na Emanuel Okwi wa Uganda.
Maana yake, ili Wabrazil hao wote wasajiliwe, Yanga SC inatakiwa kuacha mchezaji mmoja wa kigeni- wakidhi matakwa ya kanuni ya usajili kuhusu wachezaji wa kigeni.
Awali, wakati Jaja anakuja, uongozi ulikuwa katika mpango wa kumuacha Okwi, kwa sababu kadha, kubwa nidhamu yake.
Okwi ni mchezaji msumbufu, huchelewa kujiunga na timu anapokwenda kwao mapumzikoni.
Zaidi, aliingia katika mgogoro na uongozi wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu, kiasi cha kukosa mechi tano za kumalizia Ligi Kuu.
Hata hivyo, baadaye ikaelezwa, Okwi hataachwa tena, bali Mganda mwenzake, Kiiza.
Sababu haswa ya kwa nini Kiiza ataachwa haikuelezwa- maana yake klabu hiyo imeona Jaja ni bora zaidi ya Diego wa Kampala.
Lakini Yanga SC wanapaswa kujiuliza, wameona wapi ubora wa kiuchezaji wa Jaja unaozidi uwezo wa Kiiza au Okwi, hadi wanataka kufikia uamuzi huo?
Yanga wanajua uwezo wa Kiiza na amekuwa mfungaji muhimu na tegemeo wa timu kwa kipindi chote cha kuwa na klabu hiyo, anaelekea mwaka wa nne sasa.
Kwa Kiiza, wakati wa kazi ni wa kazi, hana usumbufu. Nidhamu yake ya ndani na nje ya Uwanja imeendelea kumfanya awe miongoni mwa wachezaji bora wa kigeni katika Ligi ya Tanzania.
Huyo ni tegemeo hata la timu yake ya taifa, Uganda The Cranes. Kwa ujumla, Kiiza si ni mchezaji anayefaa kuendelea kuwapo Yanga tu, bali hadi kwenye kikosi cha kwanza.
Okwi ana matatizo, ni kweli na hayo yalionekana tangu akiwa Simba SC kabla ya kwenda Tunisia, lakini wakati mwinginje matatizo ya wachezaji yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na mapungufu ya uongozi.
Yanga SC walitaka kumchukulia Okwi kama mchezaji tofauti na wengine kwa namna walivyokuwa wakimnyenyekea, naye akataka kujitofautisha na wachezaji wengine kwa namna alivyokuwa akiwasumbua.
Okwi ni mchezaji, mwisho wa siku anahitaji kucheza kwa kuwa soka ndiyo ajira yake, huo utoto wote ambao amekuwa nao kwa kpindi cha chote wazi sasa unalekea ukingoni, kwa sababu hata umri unaenda.
Kikubwa, anatakiwa kuwekwa chini, kuwekewa utaratibu na kuambiwa umuhimu wa kufuata Mkataba wake unavyoelekeza.
Lakini kocha wa sasa Yanga SC, Marcio Maximo anafahamika ni asiyependa mzaha, na Okwi anajua kwa sababu alikuwepo Simba SC wakati Mbrazil huyo anafundisha Taifa Stars.
Kama Yanga SC itamchukulia Okwi sawa na wachezaji wengine, binafsi nina matumaini sana atabadilika na kucheza mpira na kikubwa ambacho naweza kuthubutu kusema kuhusu Mganda huyo, ndiye mchezaji mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kigeni kati ya waliomaliza msimu uliopita.
Sijui wapya waliokuja akina Coutinho, Jaja, Ismaila Diara wa Mali, Leonel Saint- Preux wa Haiti wa Azam FC na Pierre Kwizera wa Simba SC kutoka Burundi kama miongoni mwao atatokea wa kumfunika Okwi.
NANI WA KUTEMWA?
Ukweli ni kwamba Yanga SC inakabiliwa na mtihani wa kukata mchezaji mmoja ili kukidhiti matakwa ya kanuni ya wachezaji wa kigeni.
Kwa sasa Maximo ameelekeza nguvu katika mazoezi ya kuijenga miili ya wachezaji zaidi, bado hawajaanza kuucheza mpiea kisawasawa hivyo hata kama Jaja na Coutinho wangekuwa majaribioni, wangefuzu kwa kigezo kipi?
Hawa Wabrazil wa Yanga wanatakiwa kupata mechi japo mbili wacheze, ili kidogo uwezo wao uonekane na ulinganishwe na wachezaji waliopo kabla ya kuamua nani aachwe.
Uamuzi mwingine wowote wa kutaka kukata mchezaji hata kabla ya kujiridhisha na uwezo wa wachezaji wapya ni wa hatari.
Azam wamemvunjia Mkataba na kumlipa Mganda Brian Umony kwa sababu ya Diara kutoka Mali- na tayari wameanza kujuta. Wamegundua mchezaji mpya hafikii hata robo ya uwezo wa mchezaji aliyendoka na tayari wamekwishatoa mamilioni kibao ya kumpa Mkataba.
Lakini si Mali ndiko anakotokea Saydou Keita na mafundi wengine kama Frederic Kanoute, iweje Diara awe mbovu? Sasa na Yanga wanendelee kujidanganya, Brazil anatokea Pele, Romario, Ronaldo, Ronaldinho na Neymar basi wachezaji wote huko ni wazuri.
NINI CHA KUFANYA?
Yanga ilimaliza Ligi Kuu kama timu bora msimu uliopita licha ya kuzidiwa kete na Azam FC katika mbio za ubingwa.
Wajuaji watatu waliikosesha ubingwa Yanga SC na vizuri wamekwishawekwa kando sasa kwenye masuala ya timu- kinyume cha hapo, timu hiyo ingetetea taji, tena kwa kishindo.
Baada ya msimu Yanga ilipoteza mshambuliaji mmoja wa kigeni, Didier Kavumbangu na kiungo mzalendo Frank Domayo waliohamia Azam FC na wachezaji wanaotaka kusajiliwa ni kiungo na mshambuliaji kutoka Brazil.
Tatizo tu ni kwamba, wapya wote wote wa kigeni wakati aliyeondoka mmoja ni mzalendo.
Jambo la kufanya kwa Yanga hivi sasa, kwanza ni kuangalia uwiano wa wachezaji katika nafasi na ubora wao, ili ikibidi kukata mgeni mmoja, basi ijiridhishe anayekatwa amestahili.
Kwa ujumla viungo walioondoka Yanga ni wawili, Domayo na Athumani Iddi ‘Chuji’, lakini pia Omega Seme amerudishwa kikosini, wakati Salum Telela amepona, Hassan Dilunga bado yupo na Niyonzima pia mipango mipya ni Mbuyu Twite kuchezeshwa kama kiungo mkabaji.
Washambuliaji baada ya kuondoka Kavumbangu, wanabaki Okwi, Kiiza, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Jerry Tegete na ameongezeka Jaja.
Bado kuna winga mwenye kasi, Mrisho Ngassa ambaye anaweza kucheza pia kama mshambuliaji wa kati.
Yanga ihakikishe inaingiza mtu mpya mwenye uwezo kuliko hawa waliopo, ili kukwepa kusajili kama fasheni. Coutinho anaweza kuwa bora kuliko Haruna Niyonzima? Jaja anaweza kuuzidi uwezo wa Kiiza na Okwi? Mechi mbili tu za majaribio Uwanja wa Taifa, zitatosha kutoa majibu, Yanga wasiamue mezani masuala mazito kama haya. Wawashirikishe mashabiki wao Taifa. Ramadhani Karim.

.png)
0 comments:
Post a Comment