Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji amepata dili lingine katika orodha ya biashara zake- baada ya kupewa mkataba wa kusambaza bidhaa za kampuni inayoongoza ya magari nchini India, Mahindra & Mahindra.
M&M ya India leo imezindua magari yake mapya mawili, Dar es Salaam pamoja na kuitangaza kampuni ya Jolly Enterprises Limited kuwa msambazaji wa bidhaa zake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika ofisi za Jolly, barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa M&M Mashariki ya Kati na Afrika, Sanjay Parab alisema kwamba wanayo furaha kuingia uhusiano na kampuni hiyo.
Amesema Jolly Enterprises ni kampuni tanzu ya kampuni maarufu nchini, Quality Group Limited ya Tanzania inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji.
Pamoja na kuitambulisha Jolly Entertainment kama msambazaji wa bidhaa zao nchini, Parab alizindua gari jipya la M&M lijulikanalo kama XUV-500 linalouzwa kwa dola za Kimarekani 46,0500, zaidi ya Sh. Milioni 75,000 za Tanzania.
Pia alitambulisha gari lingine jipya katika orodha ya magari yaliyotengenezwa na kampuni hiyo, ambalo ni Mahindra Genio na kwamba zote tayari zipo katika soko la Tanzania.
Magari mengine maarufu ya M&M yaliyopo sokoni ni Scoripio SUV, Mahindra Pick Up, Bolero Pich Up na Maxximo.
Ofisi za Jolly zipo barabara ya Nyerere, karibu kabisa na jengo la Quality Group na tayari gari mbalimbali zinazotengezenewa na M&M zipo kwenye duka lao.
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji amepata dili lingine katika orodha ya biashara zake- baada ya kupewa mkataba wa kusambaza bidhaa za kampuni inayoongoza ya magari nchini India, Mahindra & Mahindra.
M&M ya India leo imezindua magari yake mapya mawili, Dar es Salaam pamoja na kuitangaza kampuni ya Jolly Enterprises Limited kuwa msambazaji wa bidhaa zake.
![]() |
Gari jipya aina ya SUV 500 likizinduliwa leo ofisi za Jolly Entertainment |
![]() |
Meneja Mkuu wa M&M Mashariki ya Kati na Afrika, Sanjay Parab akizungumza wakati wa uzinduzi |
![]() |
Hili ndilo gari lenyewe, linaweza kuwa lako kwa dola 45.0600 za Kimarekani |
![]() |
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria uzinduzi huo |
Amesema Jolly Enterprises ni kampuni tanzu ya kampuni maarufu nchini, Quality Group Limited ya Tanzania inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji.
Pamoja na kuitambulisha Jolly Entertainment kama msambazaji wa bidhaa zao nchini, Parab alizindua gari jipya la M&M lijulikanalo kama XUV-500 linalouzwa kwa dola za Kimarekani 46,0500, zaidi ya Sh. Milioni 75,000 za Tanzania.
Pia alitambulisha gari lingine jipya katika orodha ya magari yaliyotengenezwa na kampuni hiyo, ambalo ni Mahindra Genio na kwamba zote tayari zipo katika soko la Tanzania.
Magari mengine maarufu ya M&M yaliyopo sokoni ni Scoripio SUV, Mahindra Pick Up, Bolero Pich Up na Maxximo.
Ofisi za Jolly zipo barabara ya Nyerere, karibu kabisa na jengo la Quality Group na tayari gari mbalimbali zinazotengezenewa na M&M zipo kwenye duka lao.
0 comments:
Post a Comment