• HABARI MPYA

    Thursday, August 07, 2014

    MAN UNITED NA BAYERN MUNICH ZA MAGWIJI KUKUMBUSHIA FAINALI LA LIGI YA MABINGWA 1999

    MAGWIJI wa Manchester United, Paul Scholes, Bryan Robson ana Edwin van der Sar ni baadhi ya wachezaji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu watakaocheza mechi ya hisani dhidi ya nyota wenzao wa kitambo wa Bayern Munich Jumamosi.
    Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Allianz Arena, itashuhudiwa mabingwa wa sasa wa Bundesliga wakimenyana na wakali wanzao wa enzi hizo wa United.
    Timu hizo mbili zilikutana katika mechi kadhaa enzi zao, lakini zaidi mpambano ambao bado upo kwenye kumbukumbu za wengi ni wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999, ambayo United ilishinda katika msimu waliotwaa mataji matatu. 

    Mido kisheti: Paul Scholes ni miongoni mwa wachezaji wa Manchester United wa zamani watakaocheza dhidi ya magwiji wa Bayern Munich katika mechi ya hisani Uwanja wa Allianz Arena Agosti 9
    Memorable: Manchester United beat Bayern Munich 2-1 in 1999 to win the Champions League
    Kumbukumbu: Manchester United iliifunga Bayern Munich 2-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1999

    Paul Breitner - aliyeiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1974 atakuwa Nahodha wa Bayern Munich ambayo itakuwa pia na wakali kama Marc van Bommel  na kiungo wa zamani wa United, Owen Hargreaves.
    Kikosi cha United pia kitahusisha wakali wa zamani kama Dwight Yorke, Andy Cole, Ronny Johnsen na Quinton Fortune. Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Nina uhakika litakuwa tukio moja maalum sana,".
    Fedha zitakazopatikana katakana na mauzo ya tiketi zitakwenda katika mfuko wa kituo cha watoto cha Allianz.
    Poacher: Andy Cole (left), who played for Manchester United in the 1999 final, will appear for the Reds
    Muuwaji: Andy Cole (kushoto), aliyeichezea Manchester United katika fainali ya mwaka 1999 atakuwepo pia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED NA BAYERN MUNICH ZA MAGWIJI KUKUMBUSHIA FAINALI LA LIGI YA MABINGWA 1999 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top