• HABARI MPYA

    Friday, August 22, 2014

    NUSU FAINALI KAGAME LEO, NI APR AU POLISI KWENDA FAINALI LEO?

    Na Nagma Khalid, KIGALI
    NI vita vya wenyewe kwa wenyewe ndio neon jepesi kwenye mechi ya leo inayowakutanisha wanyeji wa mashindano hayo timu ya APR  na Polisi katika mchezo wa nusu fainali.
    Mchezo huo umevuta hisia za mashabiki wengi jijini humu kufuatia upinzani uliopo ikiwa pamoja na kujuana udhaifu wao kiundani zaidi.
    APR yenye mashabiki wengi iliingia hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kumtoa mpinzani wake Rayon Spots katika hatua ya robo fainali huku Polisi ikitinga hatua hiyo kishujaa kwa kumfunga  Atletico ya Burundi.
    Nyasi za Nyamirambo zitawaka moto leo

    Kocha wa APR, Petrovic Ljubomir alizungumzia mchezo huo kwa kusema anajuana  wapinzani wao Polisi hivyo atatumia udhaifu wao ili kuibuka na ushindi mnono.
    Alisema anakiamini kikosi chake kuwa kitaweza kuonyesha maajabu ya kucheza Fainali na kulibakisha kombe hilo nchini  Rwanda ambapo ndipo mdhamini kuu anaishi.
    Nae Kocha wa Polisi, alisema anatambua umuhimu wa mechi hiyo hivyo hatafanya mzaha kuhakikisha timu yake inaibuka na ushindi mnono kwenye mechi hiyo.
    “Hii mechi ni muhimu sana kwetu, hivyo najua APR ina mashabiki wengi ila nitapambana kuhakikisha tunaibuka na ushindi mmono,”alisema.
    Mbali na mechi hiyo leo pia kutakua na mechi kati ya KCCA ya Uganda na El Merreikh walioitoa Azam katika Uwanja huo huo wa Nyamirambo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NUSU FAINALI KAGAME LEO, NI APR AU POLISI KWENDA FAINALI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top