• HABARI MPYA

    Saturday, August 02, 2014

    SIMBA SC KUKUTANA POLISI KESHO, AJENDA 13 MEZANI, HATIMA YA WAMBURA ITAJULIKANA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu kesho katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.
    Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wanachama wote wa klabu hiyo wanatakiwa kuhudhuria.
    Kaburu amesema ajenda za Mkutano huo ni 13 na kwa umuhimu wake ni vyema wanachama wote wakahudhuria.
    Makamu wa Rais wa SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'
    Amezitaja ajenda hizo kuwa ni Uhakiki wa wanachama wanaostahili kuhudhuria Mkutano Mkuu, kuthibitisha ajenda, kuthibitisha kumbukumbu za Mkutano uliopita na yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita.
    Ajenda nyingine alizozitaja Kaburu ni Hotuba ya Rais (Evans Aveva), kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Utendaji, Kuthibitisha Bajeti ya Mwaka na Kuthibitisha Uteuzi wa Wakaguzi wa Hesabu wa Nje.
    Kaburu amesema ajenda nyingine ni Uteuzi wa Walezi na Wadhamini wa klabu, Marekebisho ya Katiba, Hatima ya wanachama 72 waliosimamishwa na Kamati ya Utendaji Michael Wambura, Wanachama wa Heshima na kufunga kufunga Mkutano.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC KUKUTANA POLISI KESHO, AJENDA 13 MEZANI, HATIMA YA WAMBURA ITAJULIKANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top